POGBA AINGIA ANGA ZA PSG, WAMUUNGANISHA NA DI MARIA

POGBA AINGIA ANGA ZA PSG, WAMUUNGANISHA NA DI MARIA
KLABU ya Paris St Germain Inaelezwa kuwa imetuma ofa k
wa Manchester United ili kupata saini ya kiungo mshambuliaji Paul Pogba.

Pogba mwenye miaka 27 amekuwa akihusishwa kujiunga na PSG pamoja na Real Madrid ambazo zinahitaji saini yake.

PSG wameunganisha na ofa ya kiungo wao mwenye miaka 32 Angel di Maria ambaye aliwahi kusajiliwa na Manchester United.