TIPWATIPWA TETEMA... OOH TETEMA!- 28
ILIPOISHIA:
Nilivuta picha na kujiona nikiwa nimekonda sana, mwili mzima ukiwa na vidonda na nikikohoa sana kutokana na maambukizi ya Ukimwi, mapichapicha ya majeneza, watu wakiwa msibani na misalaba makaburini yakawa yanapitapita kwenye kichwa changu na kuzidi kunipagawisha.
“Hebu ngoja kwanza, dereva hebu simama!” nilisema kwa sauti ya juu, Jack akanigeukia kwa mshangao.
SASA ENDELEA...
“Vipi tena?”
“Nimepigiwa simu kuna dharura nyumbani! Wewe nenda mimi nitakuja siku nyingine,” nilimwambia huku nikiwa tayari nimeshasimama na kwa kuwa nilikuwa nimepanda upande wa mlangoni, Bajaj iliposimama tu, niliruka na kuzunguka upande wa nyuma, nikavuka barabara mbiombio huku nikikoswakoswa na magari na bodaboda.
“Chandeee! Una nini wewe?” aliita Jack kwa sauti ya juu lakini tayari alishachelewa, daladala iliyokuwa inatokea upande wa Shekilango ikielekea Makumbusho ilikuwa imenikaribia, nikaipungia mkono, ikasimama! Nikajichoma ndani na safari ikaanza huku nikigeuka kumtazama Jack na yule dereva wa bodaboda ambao walikuwa wamepigwa na butwaa.
Niliwaona wakigeuza Bajaj na wakawa wanaifuata ile daladala yetu kwa nyuma, Jack akawa ananipigia simu yangu, nikapokea.
“Mbona sikuelewi Chande!”
“Nimepigiwa simu Jack! Nyumbani kuna matatizo.”
“Muongo! Muda wote upo na mimi mbona sijaona simu yako ikiita?”
“Imeita Jack, kweli tena.”
“Unakimbia kwenda kupima si ndiyo?”
“Ha...pa...na! Sijakimbia.”
“Kwa hiyo kumbe wewe unajijua una ngoma ulikuwa unataka kuniambukiza si ndiyo?”
“Mimi sina ngoma Jack! Kweli tena, huwa natumia kinga,” nilidanganya huku nikitetemeka. Hofu ya kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ilinifanya niwe mithili ya kifaranga cha kuku kilicholowanishwa na mvua.
“Sasa sikia! Najua hujapigiwa simu wala nini ila umekwepa kupima ngoma! Nakupa nafasi ya mwisho, shuka kwenye daladala sisi tupo nyuma yako, mguu wangu mguu wako mpaka hospitali tukapime. Ukikataa kwenda kupima leo basi naomba usinitafute tena.”
“Nitakuja Jack lakini siyo sasa hivi! Nakuomba unielewe! Nitakuja, kweli tena, siyo kwamba naogopa kupima,” nilisema lakini Jack akakata simu akionesha kupandwa na jazba. Mbele kidogo niliishuhudia ile Bajaj ikigeuza na kurudi kule ilikotoka, nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye siti yangu.
Kumbe wakati naongea na Jack, nilikuwa naongea kwa sauti ya juu kiasi cha kufanya abiria wengine wote wawe wananitolea macho huku wengine wakibonyezana. Nikasikia wengine wakianza kucheka chinichini huku wakinitazama kwa macho ya kuibia.
“Vipi kijana, unaogopa kupima ngoma? Inaonesha una mambo mengi wewe.”
“Aah! Hamna mzee, huyu dada anataka kunichanganya.”
“Sasa unaogopa nini? Si bora ukapime ili ujue moja! Siku hizi kuna dawa na ukifuata masharti unaweza kuishi miaka mingi tu, nakushauri nenda kapime,” yule mzee niliyekuwa nimekaa naye siti moja alianza kunihubiria kwa sauti kubwa, nikaona kama anazidi kuniletea ‘uchawi’.
“We mzee vipi wewe? Nakuheshimu ujue,” nilisema kwa sauti ya juu huku nikisimama pale nilipokuwa nimekaa, abiria wengine wakaanza kuchangia hoja, eti kila mtu akinishauri nikapime.
“Nyie mmepima? Mbona mnanishikia bango mimi? Kwanza sijawahi kufanya mapenzi, mimi bado mdogo,” nilisema kwa sauti ya kupaniki na kusababisha abiria wote ndani ya daladala waangue vicheko kwa nguvu.
“Hata macho yako yanaonesha kwamba wewe ni mjanjamjanja sana wa wanawake! Naona umepatikana leo, kapime kijana,” walizidi kunishambulia nikaona njia nyepesi ya kuepukana na zogo hilo ni kuteremka kwenye daladala.
“Konda shusha hapo!”
“Unashuka umefika kweli? Au ndiyo umevurugwa?” yule mzee akizidi kuniandamana, abiria wote wakawa wanacheka hawana mbavu. Daladala ilipopunguza mwendo kwa sababu ya foleni, nilienda kushuka kwa nguvu, konda wala hakunidai nauli, naye akawa anacheka sana.
“Mnapenda kuuza mechi mkiambiwa kupima mnakuwa wakali! Kapime mdogo wangu, ngoma kitu gani kwani,” alisema kondakta nikiwa nimeshateremka, nikasikia gumzo kubwa likiibuka mle ndani ya daladala, kila mtu akisema lake.
Hata sikuwa najua pale niliposhukia ni wapi, niliiona siku hiyo kuwa ya mkosi mkubwa kwangu!
Nyumbani baba mdogo anatishia kwamba akimgundua anayemlia mali zake atamuoa kisha kumchinja, Jack ananing’ang’aniza nikapime virusi vya Ukimwi, abiria ambao hata hawanifahamu nao wananishikia bango nikapime! Ama kwa hakika ilikuwa siku mbaya sana kwangu.
“Broo eti hapa ni wapi?”
“Bamaga!”
“Hapa nikitaka kwenda Kinondoni napanda magari ya wapi?”
“Panda yanayoenda Makumbusho, ukifika pale kituoni ndiyo kuna magari! Vipi mbona jasho linakutoka sana?”
“Aah! Kawaida tu,” nilimjibu kijana mmoja aliyekuwa anauza maji pale kituoni, nikawa naelekea kwenye sehemu ya kuvuka barabara ili nikapande magari ya Makumbusho kama alivyoniambia! Kichwa kilikuwa kimechanganyikiwa kabisa.
Ni hapo ndipo nilipomkumbuka yule mama niliyekutana naye kwenye daladala wakati nikimfuata Jack, nikaona anaweza kuwa msaada mzuri kwangu kwa muda huo kwani nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa.
“Haloo mama!”
“Haloo mwanangu! Umefika Mori?”
“Nimefika mama na sasa narudi! Nilikuwa nataka kuonana na wewe, ulisema nitakupataje?”
“Hapo ulipo kuna dereva yeyote wa bodaboda?”
“Ndiyo!”
“Hebu mpe simu niongee naye!” aliniambia, nikamsogelea dereva mmoja wa bodaboda ambaye baada ya salamu, nilimpa simu, akawa anaongea na yule mama.
Je, nini kitafuatia? Usikose sehemu ya mwisho! Jiandae kuendelea na Saa za Giza Totoro (The Darkest Hours!)

πWAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO