TCRA: EPUKENI KUANDIKA HABARI ZENYE MIHEMKO NA ZENYE MAONI BINAFSI
Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Rolf Kibaja ,akizunguza na wanahabari kuacha mihemko badala yake waandike habari zenye ulinganifu.
Baadhi ya waandishi walioshiriki katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA)
Wakwanza kulia ni makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wahabari mkoani Arusha Musa Juma akiwa pamoja na waandishi wengine waliohudhuria semiana hiyo ya siku moja
Na.Vero Ignatus,Arusha
Wito umetolewa kwa waandishi wa habari juu ya kanuni mpya zilizoongezwa kwenye sheria mpya ya EPOCA, pamoja na kuacha kufanya shughuli zao kwa ushabiki hiyo, itasaidia kuwapa wanachi taarifa zilizofanyiwa kazi na ambazo zipo katika mlengo sahihi.
Akizungumza mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha Cloud Gwandu katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na APC kwa kushirikiana na TCRA kwa wanahabari ,alisema kuwa ni vyema wakahakikisha kuwa, shughuli zote wanazozifanya za uandishi ziwe zinaendana na sheria kanuni na taratibu zote walizowekewa .
Gwandu aliwashukuru Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA)na kusema kuwa mwandishi anahitajika kupewa elimu ,na kumbushwa masuala yanayogusa moja kwa moja ,katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku
Akizungumza Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Rolf Kibaja ,aliwataka wanahabari kuacha mihemko badala yake waandike habari zenye ulinganifu,mizania na kwa uafasaha sambamba na kujiepusha na maoni yao binafsi
Kibaja aliwakumbusha waandishi kuwa Tume ya uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kutoa matokeo ya uchaguzi ,na siyo wao kujitwika majukumu ambayo siyo ya kwako,alisisitiza endapo kutakuwa na tashwishwi yeyote ni vyema wakapata majibu sahihi kutoka kwa tume yenyewe
Aidha aliwasihi kuzingatia na kufuata kanuni na maadili maudhui mtandaoni ,pamoja na kuhakikisha habari kabla haijapelekwa kwa walaji lazima iwe na usawa pande zote mbili, ili kuleta tija katika jamii bila kusahau kuzingatia kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2020 namba 343.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani Arusha Musa Juma, aliwasilisha mada isemayo usalama wa waandishi kazini na mitandao ya kijamii ,ambapo alisema kuwa mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake, hivyo aliwataka wanahabari kuacha kuweka taarifa zao muhimu katika mitandao hiyo ,kwani ni rahisi mtu yeyote kuwafuatilia na hata kudhurika pia
Aliwataka kufahamu kuwa kwa miaka ya sasa ni vigumu sana kuishi bila kutumia intaneti ,kwa namna moja ama nyingine bali intaneti hiyo ina madhara pia ,kwa mfano: kukumbana na taarifa za uongo,kichaka cha uhalifu, hurahisisha udanganyifu wa taaluma,pia ni chanzo cha kusambaa kwa virusi vya kompyuta.
Musa alisema kuwa mitandao hiyo ikitumika vizuri zipo fursa mbalimbali za kufungua milango mipya ya chombo kingine cha habari,pia imeweza kuwaleta watu wengi kwa karibu zaidi ila tahadhari ni muhimu mno ,haswa kwa waandishi kwani maisha yao yana thamani kubwa kuliko kitu chochote kile ,hivyo ni vyema wakaitumia kwa umakini wa hali ya juu.
Hivyo aliwataka waandishi wa habari kutawala matumizi yao pamoja na kuzingatia kanuni za usalama kwenye mitandao ili wasiathirike .