RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. ALI MOHAMED AMEWAONGOZA WAUMINI YA DINI YA KIISLAM KATIKA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. ALI MOHAMED AMEWAONGOZA WAUMINI YA DINI YA KIISLAM KATIKA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN

 

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhajj
Dk. Ali Mohamed  Shein, akitia ubani  kumainisha kuyafungua Maulidi ya
Kuadhimisha Kuzaliwa kwa MtUME Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika
viwanja ya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar, yalifanytika jana
usiku.18-10-2020.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk. Ali Mohamede Shein akikabidhiwa Qasweeda ya Mwaka wa Kiislam1442 na Mdhamini wa Jumuiya ya Milade Nabii Association – Zanzibar Sheikh.  Sherali Champsi, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar jana usiku na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Hassan Othman Ngawi na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi.(Picha na Ikulu)

Ustadh Khamis Ali Tano kutoka Donge Mchangani Mkoa wa
Kaskazini Unguja akisoma Barzanji Mlango, wakati wa hafla ya Maulidi ya
Kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiku
18/10/2020 katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.(Picha na
Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na (kushoto kwa
Mama ) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan, wakijumuika na Waumini wa Dinui ya Kiislam katika hafla
ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad yaliofanyika katika viwanja
vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar, wakiwa wamesimama wakati
Madrassatul Qullatenia ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar wakitowa Salamu
ya Rais.(Picha na Ikulu)

WANAFUNZI wa Madrasatul Tarbiyatul Islamia kutoka Koani
Wilaya ya Kati Unguja wakisoma Qasweeda, wakati wa Maadhimisho ya 
Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad, yaliofanyika katika viwanja vya
Maisara Suleiman Jijini Zanzibar jana usiku.(Picha na Ikulu)