JIMBONI LUDEWA NI HEKA HEKA TUU,MBUNGE MTEULE JOSEPH KAMONGA AMUOMBEA KURA ZA USHINDI DKT JOHN POMBE MAGUFULI KILA KONA

JIMBONI LUDEWA NI HEKA HEKA TUU,MBUNGE MTEULE JOSEPH KAMONGA AMUOMBEA KURA ZA USHINDI DKT JOHN POMBE MAGUFULI KILA KONA

 

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa na wananchi wa kijiji cha Ludende alipokuwa akifanya mkutano wa kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM,Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akihutubia wananchi wa Kijiji cha Milo
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akipokea zawadi ya kuku aina ya jogoo pamoja na debe mbili za viazi kutoka kwa wanakijiji wa Ugera kilichopo katika kata ya Mkongobaki.
Vijana wa maigizo wakionyesha mfano wa mafiga matatu wakimaanisha wachague viongozi wa chama cha Mapinduzi kuanzia Rais, Mbunge pamoja na Diwani.
Mbunge mteule jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa amemuinua juu kuku aina ya jogoo baada ya kukabidhiwa zawadi na wakazi wa Kijiji cha Madundo kata ya Ludende wilayani Ludewa.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa na diwani mteule wa kata ya Ludende
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akikabidhiwa zawadi ya mkungu wa ndizi pamoja na mbuzi na viongozi wa Kijiji cha Mkongobaki kilichopo katika kata ya Mkongobaki wilayani Ludewa baada ya kumaliza mkutano wa kumuombea kura Rais John Pombe Magufuli.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (Mwenye shati la kijani) akiwa amekaa na wananchi wa kijiji cha Milo kata ya Milo alipowasili kufanya mkutano katika eneo hilo
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisalimiana na wananchi waliomsimamisha njiani kwa lengo la kumsalimia
Bibi aliyefahamika kwa jina la Mariam Luoga mkazi wa kijiji cha Ludende akimkumbatia kwa furaha mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipowasili kwenye mkutano wa kumuombea kura Rais John Pombe Magufuli katika Kijiji hicho.