ADC waendelea kupeperusha vipaumbele vyao vitatu
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita Chama cha ADC Queen Sendinga,ameendelea na kampeni zake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na tume ya uchaguzi huku akiendelea kusisitiza vipaumbele vitatu pindi watakapoweza kushika Dola.
Akizungumza na wakazi wa mji wa Njombe katika mkutano wake uliofanyika eno la stendi ya zamani,amesema vipaumbele vyake ni elimu,afya na kilimo huku wakianza na elimu kwa kuwa ni ufunguo wa maisha.
"Vipaumbele vyetu.Cha kwanza elimu,afya na kilimo na tumetanguliza elimu kwa kuwa ni ufunguo wa maisha,kwasababu unapomnyima binadamu elimu unampa umaskini wa akili mwili mpaka roho"Queen Sendinga
Amesema serikali iliyopo madarakani imekuwa ikitangaza kutoa elimu bure lakini bado katika utekelezaji wa adhma yao umekuwa na changamoto kubwa."Tunaambiwa elimu ya Tanzania ni bure,hakuna bure hapa tunapigwa changa la macho.Imetolewa ada mashuleni bado kumebaki michango,kumebaki mzigo kwa wazazi kununua vitabu"alisema Queen Sendinga
Aliongeza kuwa "Chama cha ADC kama tutapata ridhaa ya kuongoza nchi ya Tanzania,kwanza tunakwenda kubadilisha mitaala katika mfumo wetu wa elimu ili mitaala iweze kuwa rafiki"aliongeza Queen Sendinga
Kuhusu swala la maji mkoani Njombe amesema "Njombe hapa maji yanatiririka kule kwenye maporomoko wanashindwa kuwa wabunifu kuwapelekea wananchi maji majumbani,na kila uchaguzi wanakuja kuwaomba kura"Queen Sendinga
Aidha ameendelea kusisitiza swa la amani kuelekea siku ya uchaguzi"Tuna shida sawa lakini bado tuko kwenye amani,uvumilivu huu tuendelee nao na mtunze amani tuliyonayo kwa ghalama yoyote ile ili tuweze kupata mafanikio,tusidanganywe na mtu kuandamana,kushika mawe,kubeba panga kwasababu hakukupi maisha bora zaidi ya kufanya maamuzi kwenye boksi la kura"Queen Sendinga
Naye mwenyikiti wa vijana taifa wa chama hicho amewataka watanzania kufanya mabadiliko kwa kuwa inawezekana kwa kuwa bado nchi ina maadui watatu ambao ni umasikini,maradhi na ujinga.
"Kuna sababu gani ya kukumbatia chama cha mapinduzi wakati watanzania wanakusanyiwa kodi zao na isiwe sehemu ya kuondoa kero na changamoto zinazowakabili ili waweze kupata matibabu,serikali ya ADC ni miongoni mwa vipaumbele vyake vikubwa ni afya ya mtanzania"alisema mwenyekiti wa vijana
Baadhi ya wakazi mjini Njombe waliofika katika mkutano huo wameahidi kwenda kuchagua viongozi watakao wafaa na kulifikisha taifa pale wanapohitaji kimaendeleo.