MTIBWA SUGAR YAFUNGA KAZI NA MAJEMBE NANE

MTIBWA SUGAR YAFUNGA KAZI NA MAJEMBE NANE

 


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umefunga pazia la usajili kwa kusajili majembe mapya ya kazi nane kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21.


Dirisha la Usajili lilifunguliwa rasmi Agosti Mosi na limefungwa Agosti 31. Limedumu kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua mipango mingi.


Hesabu kubwa za Klabu ya Mtibwa Sugar ni kuifuta rekodi mbovu ya msimu wa 2019/20 ambapo ilimaliza Ligi Kuu Bara ikiwa  nafasi ya 14 na pointi 45 jambo ambalo halikuwahi kuwakuta ndani ya misimu 10 mfululizo. 


Nyota ambao imemalizana nao ni pamoja na beki wa kati Geoffrey Luseke na kiungo Juma Nyangi waliokuwa Alliance FC, Baraka Majogoro kiungo kutoka Polisi Tanzania, George Makanga kutoka Namungo.


Abal Kassim kutoka Azam FC yeye ni kiungo, Hassan Kessy kutoka Nkana FC ya Zambia yeye ni beki wa kulia, Abubakari Ame yeye ni beki kutoka Klabu ya Malindi ya Zanzibar na Ibrahim Hamadi yeye ni mshambuliaji kutoka Klabu ya Zimamoto ya Zanzibar.