Ebu litambue hili vyema ni muhimu sana kuelekezea nguvu zako, muda wako na upendo wako kwa anayekupenda.. Hapa nina maana kwamba mpende anayekupenda asiyependa achana naye.
Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio mungu wa kukufanya atakavyo.
Ndiyo asiyekupenda huwezi ukaona anapoteza muda na wewe kwenye mambo ya msingi ya kimaisha ila utaona tu hisia zikimzid huko ndio anapiga simu nyingi nyingi na kujidai mtulivu na mwenye mapenzi siku hiyo hadi washangaa
Unajua nini my dear? Nikwambie hivi.
Muache aende .. Unalala, haupati usingizi juu ya mtu ambae huenda amelala na mtu mwingine muda huu kwa amani tele...muache aende!
Unaangalia simu yako sasa hivi ukisubiri text ya mtu ambae unamuona yuko online anachati na mtu mwingine kwa furaha zote...muache aende!
Unaweka status za huzuni watsapp kuonesha namna gani unavyoumizwa, wakati yeye yuko busy anamfikiria mtu mwingine, anampa furaha mtu mwingine, anamuweka status kuwa anampenda sana na wewe amekuficha usiweze kuiona status.
Muache aende..! Kweli unalia juu ya mtu ambae anamfurahisha mwingine?? Sio sawa kabisa, hebu sikiliza, kama wewe siye ambaye anakujali, basi hutakiwi kuwa na wasiwasi tena, wewe siye wake. Yuko mtu mwingine badala yako.
Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi nyani kwamba asali ni tamu kuliko ndizi...muache aende!
Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...muache aende!
Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu..muache aende!
Cha kujifunza ni hiki
Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!
Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano. Kwani aliyesema mahusiano lengo lake kukondeshana na kutoana machozi kama mtu unapika ugali wa vitungu ni nani? Ebu muache aende
Nikutie_moyo: usivunjike moyo, inuka na endelea.. "pause and remember nothing lasts forever. Better days are coming, but they will come faster with faith"