Kwenye mahusiano yapo ya kuvumilia, lakini siyo haya

Neno uvumilivu lisitumike vibaya kiasi cha kuharibu mfumo wako wa maisha.. Kuna mengine hayavumiliki zaidi ya mara moja.. Kuna tabia zenye kuumiza na kukera unapo vumilia unafuga ubovu.

Ukiona mtu mpenzi au rafiiki yako havumiliki kwa tabia zake usiogope kukaa nae mbali.. Huwezi vumillia kupigwa au kutukanwa hadharani. Huwezi vumilia mpenzi kukusaliti zaidi ya mara mbili zote anasema shetani alimpitia tu..alimpitia waende wapi?

Huwezi endelea kuvumilia mtu asiye kuheshimu wala kukusikiliza hata mambo ya msingi.

Kumbuka, Siku zote anaye penda na kujali sana katika mahusiano ndiye anayeishia kuumia. Wanasema mwenye upendo wa dhati hana bahati...unaweza mpenda sana mtu naye akajua ila yeye atapuuza hisia zako na kwenda kwa mwingine au kukusumbua makusudi akiamin kuwa huwezi muacha.

Anapo taka kuachana nawe kamwe usimlazimishe kamwe abaki kwako. Kuna wakati bado una mhitaj ila yeye ameamua kuachana nawe huenda ameona amempata bora zaidi yako au amechoshwa na tabia zako. Nikwambie kitu muache aende huwezi zuia mafuriko japo ni kweli inauma kuachwa na unaye mpenda lakini yapokee maumivu leo ili kesho uishi kwa furaha na amani pasipo yeye. Ukilazimisha abaki kwako wakati yeye anataka kuondoka kesho atakuumiza zaidi na kusema wewe ndo umemlazimisha kubaki.

Kama ulishamuwekea malengo ngumu sana kumtoa akilini mwako ila utalazimika ufanye hivyo kwa faida yako... Amin kuwa yeye sio mwanaume au mwanamke pekee duniani.. Kuna sehemu yupo kwa ajili yako ndiye atae kuwa furaha na faraja yako.

Uzuri wake au pesa zake zisikufanye umlilie anapo taka kukuacha. Hapo ulipo bado unayo nafasi kumpata atakaye ogopa kukupoteza. Huyo hukuwa katika malengo yake ila yupo atakae timiza ndoto zako kuitwa baba au mume ama mke.

Hakuzaliwa kwa ajili yako..yupo wako huenda naye analia na kuumizwa  kama wewe..mda utafika mtakutana na kuanzisha safair kisha kuishi pamoja.

Usiogope kupendwa kisa umetendwa/ uliachwa au kutendwa vibaya.

Unapo yasusa mapenzi kwa sababu yake yeye kukuumiza kumbuka  yeye ana wapenzi kwa nini ujitese kisa yeye?

Kuachana naye sio mwisho wa maisha bado utabaki yule yule

Kwa nini uendelee kulia ikiwa yeye kule aliko ana furaha??. Akikuona una lia na kukonda unampa jeuri ya kusema yeye ndo alikuwa nyota yako na anajipa kiburi kwa kusema huwezi kumpta zaidi yake yeye, unajua nini my dear?

Ni kweli huwezi kumpta kama yeye maana yeye si bora zadi ya wote
 hvyo muache aende na atakapokuona ukiwa na  furaha na kupendeza atajidharau na kujiona boya tu hvyo jambo la hekima inuka uendelee na safari yako.