BIASHARA UNITED KUJA NA MOTO MKALI MSIMU WA 2020/21
FRANCIS Baraza,Kocha Mkuu wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa atahakikisha timu yake inakuwa moto wa kuotea mbali kwa msimu mpya wa 2020/21.
FRANCIS Baraza,Kocha Mkuu wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa atahakikisha timu yake inakuwa moto wa kuotea mbali kwa msimu mpya wa 2020/21.
Pazia la Ligi Kuu Bara linatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Septemba 6,2020 ambapo timu ya Biashara United itaanza kumenyana na Gwambina FC.
Mchezo huo wa kwanza kwa Biashara United utawakutanisha dhidi ya Gwambina FC ambao wametoka kupanda daraja kwa msimu wa 2020/21.
Baraza amesema:"Kuna wachezaji nane wameondoka na tumesajili wachezaji saba ndani ya kikosi hivyo katika hali ya kawaida hawa wanatakiwa kuzoeana ili kwenda na kasi.
"Ligi ya msimu huu inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na namna timu zinavyojipanga lakini sisi tupo tayari tutakuja kivingine na kasi nyingine."
Msimu wa 2019/20, Biashara United ilimaliza ikiwa nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 38 na kibindoni ilikuwa na pointi 50.