BEKI BORA MSIMU WA 2019/20 APEWA TUZO NYINGINE TENA
UONGOZI wa Azam FC umempa tuzo nyingine tena beki bora wa msimu wa mwaka 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara Nicolas Wadada.
UONGOZI wa Azam FC umempa tuzo nyingine tena beki bora wa msimu wa mwaka 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara Nicolas Wadada.
Tuzo hiyo amepewa na Meneja Masoko wa Azam FC, Tunga Ally ikiwa ni sehemu ya kumpa pongezi kwa kuweza kufanya vizuri ndani ya msimu wa 2019/20.
Wadada amekabidhiwa mchoro wa picha yake uliochorwa ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa msimu uliopita.
Beki huyo wa kulia aliwapoteza mazima Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union na David Luhende wa Kagera Sugar.
Aliweza kuhusika kwenye jumla ya mabao 9 kati ya 52 yaliyofungwa na Azam FC msimu uliopita ambapo alifunga bao moja na kutoa pasi nane.
Pia Wadada raia wa Uganda kwa msimu wa 2019/20, alikabidhiwa tuzo nyingine ya kuwepo kwenye kikosi bora cha msimu wa 2019/20.