YANGA YAGONGANA NA AZAM FC ZAKUTANA KWA KIPA WA KAGERA SUGAR KUSAKA SAINI YAKE
INAELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wanamvutia kasi kipa namba moja wa Kagera Sugar, Benedickt Tinoco ili aongeze nguvu katika kikosi chao msimu ujao.
Vita yao sasa inaongezewa makali na Azam FC ambao nao pia wameshapaki basi lao ndani ya Kagera Sugar wakianza na Awesu Awesu ambaye ni kiungo aliyekuwa pia kwenye rada za Yanga.
Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza:"Yanga inafanya maboresho ya kikosi kwa sasa inahitaji kuwa na ushindani kwenye namba zote kuanzia kipa mpaka wachezaji wa ndani.
"Tinoco wa Kagera Sugar anaweza kuibuka ndani ya Yanga kwani ana uwezo mkubwa na anakubalika hivyo anaweza kuibukia Yanga siku ya Mwanachi akaendeleze kutoa changamto kwa Metacha Mnata, Faroukh Shikhalo na Ramadhan Kabwili," ilieleza taarifa hiyo.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawakuwa na msimu mzuri ndani ya 2019/20 kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao.
"Kuna mambo mazuri yanakuja kwani hatukuwa na wakati mzuri msimu huu hivyo tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao," amesema.