YANGA YAANZA NA JEMBE LA KAGERA SUGAR, INAELEZWA NI MRITHI WA TSHISHIMBI

YANGA YAANZA NA JEMBE LA KAGERA SUGAR, INAELEZWA NI MRITHI WA TSHISHIMBI


KIUNGO mkabaji wa Kagera Sugar, Zawadi Peter Mauya, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga SC.

Mauya amesaini mbele ya Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM inayoidhamini Yanga, Injinia Hersi Said, huku Kaimu Katibu wa Yanga, Wakili Simon Patrick akishuhudia.

Usajili wa kiungo huyo unakuja ikiwa ni siku chache baada ya Yanga kumpa siku 14, Papy Tshishimbi za kuamua hatma yake.


Inavyoonekana usajili wa kiungo huyo ni maandalizi kwa Yanga kujiandaa kuanza maisha mapya bila ya Tshishimbi ambaye kwa muda mrefu wamekuwa wakivutana katika suala la kusaini mkataba mpya.

Huu unakuwa usajili wa kwanza kwa Yanga kuelekea msimu ujao ambapo viongozi pamoja na wadhamini Kampuni ya GSM, wametamba kukisuka upya kikosi chao.