YANGA WAMEAMUA SASA, WAMALIZANA NA MASHINE YA KAZI YA AS VITA

YANGA WAMEAMUA SASA, WAMALIZANA NA MASHINE YA KAZI YA AS VITA

BAADA ya Yanga kukamilisha dili la winga wa AS Vita, Tuisila Kisinda, hatimaye timu hiyo imekamilisha tena usajili wa kiungo wa timu hiyo, Mukoko Tonombe.

Tonombe amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha AS Vita akicheza kama kiungo mkabaji pamoja na timu ya taifa ya DR Congo.

Chanzo chetu cha kuaminika ndani ya AS Vita, kililiambia Spoti Xtra kuwa, Yanga tayari walishamalizana na wachezaji hao ambao kwa sasa wanasubiri viwanja vya ndege nchini kwao kufunguliwa ili waweze kuwasili Tanzania.

Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, hata kama viwanja vya ndege vitaendelea kufungwa, wachezaji hao wataondoka nchini humo kwa njia ya barabara.

“Yanga walianza kumalizana na Tuisila Kisinda na baadae wakaja kumalizana na Mukoko Tonombe, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni ndege kuruhusiwa kuruka ili wachezaji hao waweze kuja huko Tanzania.

“Kwa mujibu wa wachezaji wenyewe walisema kuwa uongozi wa Yanga umewaambia kama viwanja vya ndege vitafunguliwa mapema basi watatumiwa tiketi ya ndege, ila kama itachelewa basi watatafutiwa namna nyingine ya kwenda Tanzania,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Tonombe juu ya kumalizana na Yanga, alisema: “Nipo kwenye mazungumzo na Yanga ambayo yamefikia pazuri, lakini siwezi kuzungumza jambo lingine kwa kuwa sijapewa ruhusa ya kuongea zaidi juu ya tulipofikia mazungumzo yetu.