YANGA WACHUKUA MAAMUZI MENGINE KUHUSU BERNARD MORISSON

YANGA WACHUKUA MAAMUZI MENGINE KUHUSU BERNARD MORISSON

KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Patrick Simon amesema kutokana na matukio ya Bernard Morrison ya utovu wa nidhamu amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili.

Morrison hajajiunga na timu kwa sasa ambapo mara ya mwisho kuonekana akiwa na Yanga ilikuwa ni Julai 12, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.


Baada ya mchezo huo ambapo Morrison alitolewa dakika ya 64 na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick Sibomana aliondoka jumla uwanjani na kwa sasa amekuwa akionekana akicheza mechi za mtaani huku akieleza kuwa anahofia kupigwa ikiwa anakwenda mazoezini.

“Kwanza nimeshachoka habari za Morrison lakini ni kwamba kuna kamati ya maadili ya Yanga inashughulikia suala lake muda si mrefu watalitolea maamuzi kwa sababu yametokea matendo ya kujirudia, ilibidi tumpeleke kwenye kamati ya maadili ambayo ni huru mimi sipo kwenye hiyo kamati.

“Kwa hiyo wanafanya taratibu zao wameshamwalika kumsikiliza na kufanya taratibu zao halafu watatoa uamuzi wao, sisi tunawasubiri wao pamoja na TFF watuambie maamuzi yao juu ya kesi yake. " amesema.