NIYONZIMA ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA ANUKIA AZAM FC

NIYONZIMA ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA ANUKIA AZAM FC
INAELEZWA kuwa Yanga imeamua kumpotezea kiungo anayekipiga Rwanda ndani ya Klabu ya Rayon Sports,  Ally Niyonzima baada ya kupata saini ya mbadala wake.

Awali Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo na nyota
huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Rwanda na sasa anatajwa kuingia anga za Azam FC. 

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa:"Kweli tulishaanza mazungumzo na kiungo Niyonzima ila baada ya kuipata saini ya moja ya viungo tumeamua kuachana naye.

"Ni kiungo mzuri ila tuliyempata naye ni bora pia hivyo atafanya kazi ndani ya Yanga kwa kuwa tumeshamalizana naye kila kitu," ilieleza taarifa hiyo. 

Kiungo huyo anatajwa kutua Yanga ni Zawadi Mauya ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Papy Tshishimbi raia wa Congo ambaye amegomea kuongeza kandarasi nyingine.

Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa suala la usajili kwa nyota watakaotua itawekwa wazi.