ISHU YA MAKAZI YA MORRISON WA YANGA NI PASUA KICHWA

ISHU YA MAKAZI YA MORRISON WA YANGA NI PASUA KICHWA


KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Patrick Simon amesema kuwa hawajampa makazi mchezaji wao Bernard Morrison ila wanahusika kwenye kumlipia kodi.

Morrison kwa sasa yupo kwenye mvutano na klabu ya Yanga kwenye upande wa mkataba, Morrison anadai kuwa mkataba wake ni wa miezi sita umekwisha huku Yanga wakieleza kuwa ana dili la miaka miwili.

“Morrison hatukuwa tumempa makazi ila tulimwambia atafute nyumba sisi tutalipia kwa hiyo nikisema amehama makazi nitakuwa nadanganya kwa watanzania. 

"Ambacho tunakifanya sisi kwa sasa tunamlipia kodi na mpaka sasa hivi tunafanya hivyo.”