DUCHU WA LIPULI AMALIZANA NA SIMBA, AJIFUNGA MIAKA MIWILI
DAVID Kameta,'Duchu' beki wa Klabu ya Lipuli FC inaelezwa kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba.
Beki huyo msimu huu amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Lipuli ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi saba za mabao.
Timu yake ya Lipuli imeshuka daraja baada ya kufikisha pointi 44 ikiwa nafasi ya 18 hivyo msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.