SVEN: TARATIBU WACHEZAJI WATAREJEA KWENYE UBORA

SVEN: TARATIBU WACHEZAJI WATAREJEA KWENYE UBORA


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema kuwa anaamini wachezaji wake watarejea kwenye ubora wake hivi karibuni kutokana na kuanza mazoezi ya pamoja.

Simba imeanza kufanya mazoezi tangu Mei 27 ikitumia uwanja wake uliopo Bunju ikiwa ni kwa ajili ya kujiweka sawa na kurejea kumalizia mechi za Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Juni 13 pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho.

"Wachezaji wapo vizuri na kila mmoja ninaona akiwa katika maendeleo mazuri taratibu kwani hatukuwa pamoja kwa muda mrefu.

"Kikubwa kilichopo kwa sasa ni kuendelea kufuata program zetu hatua kwa hatua kabla ya mambo kuwa sawa," amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ina pointi 71 baada ya kucheza mechi 28.