MROMANIA WA AZAM FC KUANZA SAFARI YAKE NA GARI
ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC anatarajiwa kurejea muda wowote kuanzia sasa baada ya kibali cha kuja Bongo kupatikana na ataanza kwa usafiri wa gari mpaka nchi jirani na Ujerumani kabla ya kukwea pipa kuja Bongo.
Kocha huyo kwa sasa yupo nchini Romania ambapo aliibukia huko baada ya masuala ya michezo kusimamishwa Machi 17 imekuwa ngumu kurudi mapema baada ya mipaka kufungwa.
Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa mpango wa kupata kibali kwa Cioaba umefanikiwa kinachosubiriwa ni siku ya kuja nchini. "Tayari kibali cha Cioba kuja nchini kimepatikana kwani sheria ya Romania alipo imekuwa ngumu kidogo, kocha atasafiri kwa basi kutoka hadi nchi jirani ya Ujerumani ambako ndege zimeanza kuruka. 'Muda wowote kuanzia sasa tuna uhakika wa kumpata Cioaba ndani ya Azam FC ili arejee kuendelea majukumu yake," amesema.
Azam FC imeanza mazoezi chini ya Kocha Msaidizi, Bahati Vivier huku ikiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.