LIVERPOOL YAINGIA ANGA ZA ADAMA, MWILI JUMBA

LIVERPOOL YAINGIA ANGA ZA ADAMA, MWILI JUMBA

JURGEN Klopp,  Kocha Mkuu wa Liverpool yupo kwenye hesabu za kuinasa saini ya winga mwili jumba na mwenye kasi anayekipiga ndani ya Wolves, Adama Traore.

Taarifa zinaeleza kuwa Kocha huyo anataka kuwapunguzia presha mastaa wake watatu wa mbele ambao ni Firmino,  Mo Salah na Sadio Mane.

Kwa mujibu wa The Sun, Klopp amemuweka katika kipaumbele chake cha kwanza cha usajili winga huyo mwenye miguvu na thamani yake inatajwa kuwa milioni 60.

Raia huyo wa Hispania amekuwa katika kiwango bora ndani ya Wolves msimu huu, mocha wake Nuno Espirito Santo amekuwa akimtumia zaidi pembeni.