KAGERA SUGAR YALIPIGIA HESABU KOMBE LA SHIRIKISHO

KAGERA SUGAR YALIPIGIA HESABU KOMBE LA SHIRIKISHO
UONGOZI wa Kagera Sugar unesema kuwa utapambana kwa nguvu zote ili kusepa na Kombe la Shirikisho msimu huu ili waiwakikishe nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Kagera Sugar ilitinga hatua ya robo fainali kwa kuitungua KMC penalti 2-0 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana 1-1 itakutana na Yanga hatua ya nusu fainali kati ya Juni 27/28.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema kuwa mipango yao ni kutwaa Kombe la Shirikisho ili wafikie hatua ya kuwa wa kimataifa. "Ninaiheshimu Yanga ambayo tumepangwa nayo kucheza baada ya droo ila kikubwa ambacho tunakihitaji ni Kombe la la Shirikisho ili tuwakilishe nchi kimataifa," amesema.

Kwa sasa Kagera Sugar imeanza mazoezi kujiaanda kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara ambayo ilisimama tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona na inatarajiwa kuanza Juni 13.