JEMBE LILILOTUA USIKU WA LEO SIMBA KUUNGANA NA WENZAKE MAZOEZINI

JEMBE LILILOTUA USIKU WA LEO SIMBA KUUNGANA NA WENZAKE MAZOEZINI

FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliaji wa Simba amerejea Bongo akitokea Kenya usiku wa kuamkia leo ataungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya leo yatakayofanyika kwenye uwanja wao uliopo Bunju.

Kiungo huyo alikwama nchini Kenya baada ya mipaka kufungwa kutokana na janga la Virusi vya Corona jambo lililopelekea ugumu wa safari yake.

Wachezaji wa Simba walianza mazoezi Mei 27 mara baada ya kuripoti kambini na kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Kiungo huyo ametupia mabao manne na kutoa pasi sita za mabao ndani ya Simba iliyofunga mabao 63.