REAL MADRID BADO WANAMTAKA NEYMAR JR

REAL MADRID BADO WANAMTAKA NEYMAR JR
RAIS wa Klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ana ndoto ya kupata saini ya mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr.

Neymar Jr kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kusepa ndani ya PSG ambapo ilielezwa kuwa Barcelona nao walikuwa wanahitaji kumrejesha kwenye timu yake ya zamani.

Madrid iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zinadine Zidane Inaamini kuwa Ikimpata mshambuliaji huyo Itaongeza nguvu ndani ya kikosi chake.

Msimu wa 2013-17 Neymar alikipa ndani ya Barcelona ambapo alicheza jumla ya mechi 123 na alitupia mabao 68 huku ndani ya PSG akiwa amecheza mechi 52 ametupia mabao 47.