MOUSA WAGUE BEKI WA SENEGAL ANAYEPAMBANA NA CORONA KWA VITENDO

MOUSA WAGUE BEKI WA SENEGAL ANAYEPAMBANA NA CORONA KWA VITENDO

BEKI wa kimataifa Moussa Wague mali ya FC Barcelona ambaye anakipiga kwa Mkopo Nice, ametoa tani 12 ya vyakula kusaidia jamii yao katika eneo la Bignona nchini Senegal.

Wague amesema sababu za kufanya hivyo ni kuendelea kutoa sapoti na kusaidia vita dhidi ya Virusi vya Corona.

Katika eneo hilo hadi sasa hakuna hata kisa kimoja cha Covid 19 kilicho ripotiwa lakini yeye anaamini ni vizuri kwa wakazi wa eneo hilo kuanza kujiandaa na kuchukua tahadhari.


Beki huyo anayekipiga pia timu nyake ya Taifa ya Senegal ndani ya Klabu ya Nice amecheza mechi tano huku kwenye timu ya Taifa ya Senegal ya wakubwa akiwa amecheza jumla ya mechi 18 na ametupia bao moja.