MORRISON ACHEKELEA MAISHA NDANI YA YANGA

MORRISON ACHEKELEA MAISHA NDANI YA YANGA
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morri
son amesema kuwa anafurahia maisha yake ndani ya klabu hiyo kutokana na sapoti anayopewa kutoka kwa mashabiki, wachezaji na uongozi kiujumla.

Morrison amekuwa kwenye ubora wake ambapo mchezo wake wa kwanza mbele ya Singida United alitoa pasi moja ya bao wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

"Tunaishi vizuri na kupeana sapoti kubwa kutoka kwa viongozi na wachezaji pia jambo ambalo linanifanya niwe na furaha kuwa hapa kwa sasa, maisha ni mazuri ila kikubwa kwa sasa ni muhimu kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona," amesema.

Morrison ametupia mabao matatu ndani ya Yanga Kwenye Ligi akiwa ametupia mabao matatu pia.