MADDISON AGOMEA DILI LA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

MADDISON AGOMEA DILI LA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

JAMES Maddison kiungo wa Leicester City mwenye miaka 23, amemwambia shabiki mmoja kuwa anapenda kubaki hapo licha ya kuwa imekuwa ikielezwa anawindwa na Manchester United.

Nyota huyo yupo ndani ya Leicester City ambayo alijiunga nayo msimu wa 2018 akitokea Klabu ya Aberdeen ambako huko alikuwa kwa mkopo, alicheza mechi 14 pekee na kutupia mabao mawili.

Akiwa kwenye Klabu yake ya sasa Leicester City amecheza jumla ya mechi 64 na kutupia mabao 13 anacheza pia timu yake ya Taifa ya England.