Historia Fupi ya Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani

Historia Fupi ya Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani


Na Alban Abdallah
Kwa masikitiko makubwa sana, tumepata taarifa ya msiba wa Kaka wa makaka, Retired Chief Justice, Brigadier general, the most famous Zanzibarian Christian in the Tanzanian Government History, Reverend Cannon, father, son, friend, and national hero, Augustino Ramadhani. Tunataka kutowa pole kwa mkewe, wanawe, wajukuu, na family ya Ramadhani nzima. This is a monumental loss. 

Kwa niaba ya familia yangu, nataka kumzungumzia Justice Augustino Ramadhani kama nilivomfahamu mimi. Katika bibilia, wakristo tunaambiwa tuwe chumvi ya ulimwengu (Matayo 5:13). Kaka Augustino alikuwa chumvi iliyokolea. Justice Ramadhani ndio aliyenisogeza miye binafsi kuwa karibu na kanisa. Nimeanza kulipenda kanisa, kumtukuza Mungu, na na kutaka kuwa sehemu ya kushiriki katika kuendeleza ukristo visiwani Zanzibar kwa kufata mfano wake. 
Kabla sijamaliza form 4 (1976/1977) nilikuwa narudi kwetu baada ya kucheza mpira. Nilikutana na kijana mmoja mrefu, na mkewe mrembo, wakuvutia, na mtoto mchanga aliobebwa nyumbani kwetu (Francis). Walipoondoka nilimuliza mama, wale nani? Mama akanambiya huyu ni mkristo aliozaliwa Zanzibar aliyeishi bara miaka mingi. Ameletwa Zanzibar kikazi na anapita nyumba kwa nyumba kuwasalimiye wa-Anglicana wenziwe na nujitambulisha. 
Kama kumbukumbu zangu sahihi, Marehemu Jumbe aliyekuwa Raisi wa Zanzibar alitembelea kambi ya jeshi Nachingwea. Ndipo alipokutana na Luteni wa jeshi moja alomwamkia raisi. Alivojitambulisha kwa Rais, Rais akamuliza wewe ni mtoto wa Mwalim Matthew? Akasema ndio. Rais akamuliza Justice Ramadhani, unafanya nini huku jeshini? Akamjibu, mimi ni mwanasheria. Rais akamwambia kwamba Zanzibar tuna upungufu mkubwa wa wanasheria. Baada ya muda si mrefu, Justice Ramadhani akapewa barua ya transfer kutoka jeshini na kuja kufanya kazi katika Serikali ya Zanzibar kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Na kwa wakati huo, mwasheria mkuu alikuwa Jaji Daniel Lubuva. Yeye alikuja kutoka bara pia. Kutoka hapo akaanza kazi ya kusaidia wa Zanzibari katika mambo ya sheria na hajasimama. 

Daniel Lubuva alimpeleka Pemba kwa muda mdogo na akarudishwa Zanzibar baada ya kuweka mambo sawa pemba. Rais alipotaka kumbadlisha Jaji mku wa Zaznibar (Marehemu Omar Borafya), Justice Augustino Ramadhani alichaguliwa kuwa Jaji mku wa Zanzibar. Aliweka historia kwa kuwa Jaji mku mdogo akiwa na miaka 34. Haijawahi kutokea Tanzania. 

Justice Ramadhani alianza kazi yakugeuza mahakama ya Zanzibar. Siku hizo, Ilikuwa haina utaratibu maalum wa kimahakama. Na kama historia ya Zanzibar itaandikwa siku moja, basi Justice Ramadhani ndiye aliorudisha Mahakama ya Zanzibar kuwa kama mahamakam za duniani kote. Kama kawaidi, mambo mengi hubadilika baada ya mapinduzi. Na mahakama ya Zanzibar ilibadilika kupita kiasi. Hata mahakama ikawa hairuhusu mshatakiwa yeyote kuwa na wakili wa kumtetea. Justice Ramadhani akarudisha haki za binadamu. Waziri Kiongozi wa wakati huo  (Seif Shariff Hamad) na Rais wa Zanzibar (Marehemu Abdulwakil) walisimama naye na walikubali kwamba mabadliko hayo yanahitajika.
Aliopandika barua ya kujiuzulu nafasi yake kama Jaji mkuu wa Zanzibar, alimwandikia aliyekuwa waziri wa ulinzi na jeshi lakujenga taifa Dr. Salim Ahmead Salim kumweleza kwamba Jaji Mkuu wa Zanzibar mpya atachanguliwa karibuni na yuko tayari kuendelea kufanya kazi za kuendeleza nchi yake na kusaidia wa Tanzania. Akamwomba ampangiye kazi kwa sababu yeye ni mwanajeshi alokuwa na cheo cha Colonel. Mambo hayakwenda hivo. Mungu alikuwa na mpango mwengine kwake. Aliyekuwa Raisi wa Tanzania (Alhaj Ali Hassan Mwinyi) alimteua kuwa jaji katika mahakama ya rufaa Tanzania. Hamid Mahmoud  ndiye aliyerithi nafasi ya Justice Ramadhani katika serikali ya Zanzibar, akiweka  historia  kuwa Jaji pekee aliofanya kazi ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kwa kipindi cha Zaidi ya miaka 25. 

The rest is history. Kutoka Court of Appeal Justice #4 Augustino Ramadhani kaendelea kuwa Chief Justice wa Nchi ya Tanzania (State of Tanzania). He’s one of us. Zanzibarian, Christian, Hard Working, and following God’s plan for his life. 

Turudi katika maisha yake alivokuwa Zanzibar. Mimi nakumbuka kwamba kila asubuhi akienda kazini, akirudi kwake. Na kila Jumanne na Alhamisi akija kanisani Mkunazini kufundisha kwaya. Na kila jumapili ya Mungu, akipiga kinanda kwenye kanisi kuu. Katika misa ya shangwe. Wakati huo huo, alianzisha darasa la cheti cha sheria. Akawa mwalimu anosomesha Certificate of Law wiki mara mbili kwenye shule ya taasisi ya lugha ya kigeni. Na alimwomba mwanasheria mkuu wake, Hamid Mahmoud, aje kumsaidiya kufundisha darasa hilo. Na alifanya kazi hiyo bila malipo. 

Sasa tujiulize, tunaweza kujifundisha nini katika maisha ya Justice Reverand Cannon Augustino Ramadhani? 

Mimi nitamkumbuka rafiki wangu mpenzi hivi. Hakupenda mambo makubwa kama mafundisho ya Bwana Yesu yanavyotwambiya. Hakuwa na tamaa ya mali wala vitu vya dunia hii Alikuwa na heshima ya kupindukiya. Aliheshimu wakumbwa zake na wadogo zake. Aliona umuhimu wa elimu. Maisha yake yote alitafuta wakati wakuliimarisha kanisa. 
Kila mmoja katika sisi anao uwezo wa kuiga mfano wake. Kila mmoja wetu katika sisi akifata moja ya mambo aliyofanya Justice Ramadhani, jumuia yetu ya wa Anglicana wa Zanzibar tutaona maendeleo yasokuwa na mfano. 

Bwana ametowa. Bwana ametwa. Jina la bwana lihimdiwe. Rest in Peace my dear friend. 

Alban Abdalla