BEKI HUYU WA SIMBA ATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WATUPIAJI

BEKI HUYU WA SIMBA ATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WATUPIAJI

DARUESH Saliboko, mshambuliaji wa Lipuli amesema kuwa Pascal Wawa ni miongoni mwa mabeki wagumu kupitika kutokana na nguvu, akili pamoja na mbinu zake.

Wawa anakipiga ndani ya Klabu ya Simba iliyo nchini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema kuwa kazi kubwa ya mshambuliaji ni kupenya kwenye ngome za mabeki ili kufunga ila alikuwa anapata wakati mgumu mbele ya Wawa.

"Unapomkabili Wawa ni lazima ujipange katika kasi na kuruka juu, ana mbinu nyingi ambazo ukienda kichwakichwa unaweza kukata tamaa.

"Namshukuru Mungu sina hofu katika kupambana ila ninatanguliza nidhamu kila wakati kwani mchezo wa mpira unahitaji akili na utulivu," amesema.

Saliboko ni miongoni mwa wazawa wanaofanya vizuri ametupia mabao nane ndani ya Lipuli msimu huu.