BEKI HUYU WA NKANA ANAYETAJWA KUTUA YANGA AWAPIGA MKWARA SIMBA
MUSA Mohammed, raia wa Kenya anayekipiga ndani ya Klabu ya Nkana FC amekiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.
Nyota huyo ambaye ni beki yupo huru kujiunga na klabu yeyote kwa sasa kwani mkataba wake na Nkana ya Zambia umemeguka msimu huu.
"Nimefanya mazungumzo na Yanga kupitia wakala wangu ili nijiunge nao hivyo mambo yakiwa sawa nitashuka hapo kwani ni moja ya timu zenye heshima kutokana na ukubwa wake.
"Ninayo nafasi ya kuanza kucheza kikosi cha kwanza kutokana na uzoefu wangu pamoja na uwezo siwahofii watani zao wa jadi Simba kwani ninawatambua vizuri," amesema.
Musa ni nahodha wa zamani wa Gor Mahia, aliyewahi kukipiga katika Klabu ya KF Tirana ya nchini Albania kabla ya mwaka 2018 kujiunga na Nkana ya Zambia ambayo ilikuwa ikinolewa na Beston Chambeshi.