Sababu Za Kwanini Wanaume Huumia Zaidi Wanaposalitiwa Kimapenzi Zipo Hapa.




Mapenzi ni kitu cha ajabu sana, watu kutoka koo, makabila, mataifa na wenye rangi tofauti hujikuta katika dimbwi zito. Hujikuta katika wakati ambao kila mmoja haoni kitu kingine cha thamani zaidi ya mpenzi wake. Huu ni wakati ambao si tu kuwa neno usaliti linakuwa halipo bali wapenzi hawahisi hata kama kuna maisha bila ya yule wampendaye.

Usaliti ni jambo lenye maumivu yasiyovumilika hasa ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa. Mtu hahisi kama itatokea mpaka inapotokea. Mwishoni mwa wiki hii kumeenea picha za mwanaume aliyejikatisha uhai kisa mapenzi. Hii ikanikumbusha utafiti usio rasmi nilio ahi kufanya juu ya kwanini wanaume huumizwa zaidi na usaliti kuliko wanawake.
Wanaume si wepesi kusema yaliyowasibu
Ukisikiliza vyombo vya habari au kusoma magazeti ni rahisi kukuta story ya mwanamke anayelalama baada ya mpenzi ,mchumba au mume au mume kutoka na mwanamke mwingine. Lakini ni nadra sana kukuta mwanaume akilalama! Si kwa kuwa hawaumizwi au hawana majeraha, bali ni sababu kwa wanaume inaonekana kama kujidhalilisha kusema hivyo.
Hawatamani hata rafiki zao. Huishia kuumia peke yao, huishia kuhuzunika peke yao hiyo hupelekea kujenga majeraha makubwa moyoni. Kuendelea kufuga hasira ambazo saa nyingine hupelekea wao kufanya maamuzi ya ajabu na yenye kustaajabisha kwa jamii.
Mwanaume hupenda kuendelea kuwa na nguvu juu ya jambo fulani siku zote
Ndiyo,kwa mwanaume kuwa na watu wanaomtii, wenye kumheshimu na kumsikiliza ni jambo linalompa faraja na kumfanya ajivunie. Mwanaume anapokuwa na mwanamke hupenda kuona huyo mwanamke akimnyenyekea, akimtii na kumsikiliza, Kwa taarifa yako mwanaume hapendi hata yule mwanamke asiyempenda awe wa kwanza kusema imetosha,au awe na mwanaume mwingine,inapotokea hayo humfanya mwanaume ajione amepungikiwa kitu, humfanya ahisi yeye si bora tena hapo ndipo tatizo linapoanzia.
Wanaume wana tabia ya kumuamini sana mwanamke wanayekuwa naye
Moja kati ya kazi ngumu kwa mwanamme ni kumfanya amwamini mtu mwingine kwa kiwango kikubwa, Inaweza kuchukua miaka mpaka kufikia hatua ya kumuamini mtu mwingine hasa mwanamke. Lakini inapotokea akafanya hivyo huamini jumla. Hatua ya kumuamini sana mwenza wake huleta madhara makubwa mbele ya safari. Tofauti na mwanamke ambaye siku zote anakuwa anawasha taa ya tahadhari na kujua inawezekana saa yoyote mpenzi wake atachepuka na inapotokea kweli mshtuko wake hauwezi kuwa sawa na mwanaume ambaye humwamini sana mwenza wake. Mwanamke anaweza kuzama kimapenzi au hata kuolewa na mwanaume asiye mwamini ni ngumu kwa mwanaume kufanya hivyo.
Sio rahisi kwa mwanaume kuhamisha upendo
Katika ulimwengu wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuwa wasaliti kuna msemo unasema ‘every guy cheats’ , ukweli tusioujua ni kuwa pamoja na kuwa wanaume hucheat zaidi kuliko wanawake ila wanafanya hivyo kwa sababu ya tamaa ya miili na nafsi zao hubaki kwa wenza wao wa kudumu.
Si rahisi kwa mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda na kuhamishia mapenzi hayo kwa mwanamke mwingine. Mwanamke anapokuwa mpweke Nna akatokea mtu ambaye akamtolea ule upweke anakuwa ameuwin moyo wake.
Usaliti umetokea ameamua alivyoamua, huo sio mwisho wa maisha kuna sababu nyingi za wewe kuendelea kuishi na kufurahia maisha. Pengine haya yanaweza kusaidia kukuamsha tena na kuona maisha yapo na hakuna sababu ya wewe kuumia.
Sema yanayokusibu ni dawa kuliko dawa yoyote
Kwanini uone aibu kwa kusema kama fulani amekutenda? Ni kosa lake sio lako na wala hii haikufanyi usiwe wewe ulivyokuwa juzi. Amka watafute watu waambie ni jinsi gani umeumia, toa machungu yote ya nafsini mwako,inatokea kwa watu wengi Na wewe sio wa kwanza na wala sio wa mwisho.
Usiamini kupita kiasi
Mapenzi hayazuiliki ni kitu kinachokuja na kufunika moyo wako bila taarifa sio rahisi kucontrol mapenzi juu ya mtu fulani. Lakini unaweza kucontrol kumuamini mtu mwingine. Katika dunia tuliyonayo ni nadra kupata mtu mwenye mapenzi ya dhati,usimuamini sana amini kuWa ni tabia ya wanadamu kuchoka Na kutafuta vilivyo bora zaidi. Sisemi usiamini ila siku zote amini lolote linaweza kutokea itakusaidia siku ikiwa ndivyo sivyo.
Kusalitiwa hakuondoi thamani na utu wako
Baada ya kumfanyia yote uliodhani unamfanyia ili aendelee kukupenda lakini ameondoka, roho inakuuma sababu unaona hakumbuki jinsi gani ulivyojitoa kuhakikisha ana furahi na kuwa na amani siku zote. ii haiondoi ile asili na thamani ya utu wako maisha. Ni vile tu huna habari ila yamewakuta wengi na yataendelea. Kwanini wewe uone sio mtu tena, kwanini uone labda wewe sio mwanaume tena? Kwanini uone eti pengine uanamme wako una walakini Na sio yeye ndo mjinga kwa kutojua thamani ya penzi lako.
Amini anayekuja ni bora kuliko aliyeondoka
Ambacho hukijui ni kuWa kuna wanawake mamia kwa mamia wanasubiri mwanaume wa dizaini yako atokee ili kukamilisha maisha yao. Na ni bora kuliko aliyeondoka na watathamini mapenzi yako kuliko aliyekutenda. Jipe sababu ya kuamini wewe ni kama dini lililokuwepo enzi za babu zetu likichezewa bao mpaka mkoloni alipokuja kuwaonyesha thamani na matumizi sahihi ya madini!
Hautakiwi uache kupenda, hautakiwi upunguze juhudi za kumuonyesha mtu kama unampenda. Haijalishi ni mara ngapi unaumizwa unapofanya mazuri kwa mtu fulani usitegemee kitu hicho hicho kutoka kwa huyo mtu ila amini ni hazina uliyojiwekea na kuna siku utapata thamani ya penzi uliloliwekeza.