Alikuwa na haraka mno... Sasa alifika kwenye kona fulani almanusura amgonge dada mmoja kwa haraka zake...
"ooohhh samahani dada yangu... Kwanza Assalam Aleykhum"
Suria alimsalimia mdada huyo ambaye kavaa baibui au hijabu, wengine huita nikabu.. Japo kilabu ni kile kininja...
"waaleykh msalam, haya mbona wataka nigonga na usafiri wako"
Aliongea dada huyo huku suria akiomba radhi
"niwie radhi dada yangu... Nipo katika upesi kuwahi mambo yangu"
Aliongea suria, kisha dada huyo akasema kuwa
"sawa kaka... Unaweza kwenda"
Aliongea dada huyo, lakini suria alisisimkwa na nywele zake, ikiwa na maana kuwa aliopishana nae sio binadamu wa kawaida....
lakini sasa kumbe huyu dada ndio maimati mwenyewe, mmoja wa wale majini waliokuja duniani kutafuta MWANAUME MSAFI
ENDELEA........
Qarena ni kiumbe ambaye huzaliwa na kila binadamu alioko duniani, na kiumbe hiki hakionekani na mtu yeyote, hata jini mwenyewe hakioni hiki kiumbe... Lakini kwa sauti unaweza kukisikia ila sio kwa binadamu bali ni kwa viumbe kama vile jini, wanyama na vitu vingi ambavyo viko tofauti na binadamu
Binadamu ana malaika watatu, MBELE, KUSHOTO NA KULIA... Sasa Hawa Malaika wako wa kushoto na kulia na mbele ni wazuri wote ila kila mmoja ana kazi yake.. Malaika aliopo upande wa kulia, yeye huandika matendo mazuri ambayo unayatenda duniani... Na huyu wa upande wa kushoto, yeye huandika matendo maovu ambayo unayatenda duniani hivyo hakuna tendo lako linalo potea na yote utayakuta kwa mungu... Sasa huyu wa mbele,. Kazi yake yeye ni kukuongoza njia ilio sahihi... Ila ukikataa hakulazimishi... Yeye anakupeleka kwenye nyumba ya ibada wewe unakwenda disko, huko haendi... Atakusubiri utoke ajaribu tena kukuongoza mazuri mana ndio kazi yake... Na hata hawaa waandishi wa kushoto na kulia wakiona unaingia sehemu chafu hata wao hawaingii... Sasa unaye ingia nae disko au baa, au danguro... Ama sehemu yeyote yenye starehe... Pale unaingia na Qarena, huyo ndio unaingia nae.. Afu unakutana na shetani huko huko mana nyakati hizo malaika wapo nje wakikusubiri...
Sasa huyu Qarena ndio ana urafiki na mwandishi wa kushoto ambaye anaandika matendo mabaya... Hivyo wewe ukitoka disko,.. Mwandishi wa kushoto anamuuliza Qarena yale ulio yafanya ndani, kisha anaandika mabaya ulio yafanya huko ndani... Na huyu Qarena yeye anakaa nyuma.. Ukumbuke nimetaja MBELE, KUSHOTO NA KULIA... sasa huyu Qarena yeye anakaa nyuma.. Na yeye anatunza kumbukumbu zako zote tofauti na hawa wa kushoto na kulia.. Qarena yeye anakusanya takataka zako zote ambazo unazijua,... Hakuna anayeweza kumuona Qarena ispokuwa wao wenyewe tu ndio wanaweza kuonana... Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kuona viumbe vyake.... Labda kama nawe una nafasi ya ukiumbe ndio utaweza kuona au kusikia sauti za viumbe wenzako... Au kiumbe aamue kuonekana mbele za wanadamu... Kwahio Qarena yeye anatunza kumbukumbu zako unazofanya na ulizofanya toka kuzaliwa kwako.. Na ukifa sio lazima na yeye afe, anaweza kubaki na kuendelea kuishi kwenye ukoo wenu...
SAMAHANI SANA NDUGU WASOMAJI WANGU... MIMI HUA SIPENDI MSOMAJI WANGU AWE ANAJIULIZA MARA KWA MARA NA NDIO MAANA NIKAANZA NA UFAFANUZI WA HIKI KIUME KIMBEA MBEA... HIVYO MSAMAHA MNISAMEHE, ILA NI KATIKA HALI YA KUWAELEWESHA VYEMA ZAIDI... KAMA KUNA KOSA HAPO NIMETELEZA
"sawa kaka... Unaweza kwenda"
Aliongea dada huyo, lakini suria alisisimkwa na nywele zake, ikiwa na maana kuwa aliopishana nae sio binadamu wa kawaida....
lakini sasa kumbe huyu dada ndio maimati mwenyewe, mmoja wa wale majini waliokuja duniani kutafuta MWANAUME MSAFI
JANA TULIISHIA HAPO, SASA TUENDELEE
Wakati suria kesha panda baiskeli yake na kuendelea na safari yake ya kuwahi shule ambayo anakwenda kujaribu kuomba kazi,..
ILANI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
TAHADHARI SANA KWA WEWE UNAYE UZA KAZI HII KATIKA MITANDAO YAKO YA KIJAMII...
HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA KIFUNGU CHA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MITANDAO, KWA KOSA LA KUHUJUMU KAZI ISIO YAKWAKO..
NDUGU MSOMAJI, HAKIKISHA ANAEKUUZIA SIMULIZI HII NI MMILIKI HALALI MWENYE NAMBA HII, +255714419487... LAA SIVYO NAWE NI MMOJA KATI YA WAHUJUMU WA KAZI ZA WATU, KATIKA MITANDAO YA KIJAMII.....
KWA WALE NDUGU ZANGU WA KUPOSTI KWENYE KURASA ZAO,
HAKIKISHA, UNAPATA IDHINI KUTOKA KWA MMILIKI HUSIKA KWA SIMU NO, +255714419487 WhatsApp
ILI UPEWE MAELEZO, VIGEZO, NA MASHARTI YA KUPOSTI KWENYE UKURASA WAKO WOWOTE ULE..
JIEPUSHE KUKOPI KAZI HII BILA IDHINI YA MMILIKI HUSIKA
TAFADHALI SANA HATUPO KWA AJILI YA KUPELEKANA PABAYA KISHERIA.....
TUWE MAKINI NA KAZI ZA WATU KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Sasa pale kwenye kona maimati alisita kuendelea na safari, kwani kuna kitu kahisi kwa kijana huyo..
"mkarimu, mpole, mnyenyekevu.. Atakosa kuwa msafi kweli?"
Alijiuliza maimati, bila kuchelewa papo hapo akawa invisible (isio onekana) yaani kawa upepo ghafla kisha akaanza kumfuatilia suria kule ambako anakwenda,... Yeye hatembei bali anaruka tu... Yaani anapotelea hapa anaibukia mbele.. Sasa ili maimati amfahamu vyema suria, alianza kuzungumza na Qarena
"Qarena?"
Maimati aliita japo waliitika Qarena wa watu wengine lakini maimati alikuwa jirani na suria hivyo, Qarena wa suria alijua fika anaitwa yeye
"ndio"
"pacha wako anakwenda wapi"
"anakwenda shule"
"anakwenda kufanya nini"
"kuomba kazi"
Yaani Qarena hafichi kitu,... Ukiwa na uwezo wa kuzungumza na Qarena basi utajua siri nyingi sana za watu,.. Mana qarena anajua mpaka unachotaka kukifanya..kile usichokijua basi hata yeye hajui, ila ukikijua tu na yeye keshakijua...
"pacha wako ana mke"
"hana"
"kwanini"
"sijui"
"ana mpenzi"
"hana"
"kwanini"
"sijui"
"ana mchumba"
"ndio"
"wameshafanya mapenzi"
"hapana"
"ana mchumba wa ngapi toka kuzaliwa kwake"
"ni wa pili"
"wa kwanza yuko wapi"
"sijui"
"kwanini waliachana na mchumba wa kwanza"
"waliachana kwasababu mchumba alitaka mapenzi na pacha wangu hataki"
"kwanini hataki"
"kwasababu hataki hakutaka kuchanganya mapenzi na masomo"
"pacha wako kafanya mapenzi mara ngapi toka kuzaliwa kwake"
"hajawahi"
"kuna siku anapataga shida kihisia"
"ndio, hata jana usiku kuna shetani kaja"
Yaani qarena ni mbea mpaka basi... Yaani anasema vyote,.. Mpaka jana suria kajiwa na jini mahaba, qarena kasema vyote... Maimati aliumia sana kuskia suria anatembelewaga na jini mahaba pale anapo jisahau kuomba dua...
"huko anapokwenda atapata kazi"
"sijui"
"kwanini hujui"
"yeye hajui na mimi sijui"
"anakwenda shule gani"
"SADAQ SEMINARY SEC SCHOOL"
Maimati alipotea ghafla na maeneo hayo na suria ndio alikuwa akiinga katika geti la shule hio,.. Baada ya kuingia akapaki baiskeli yake vyema kisha akaingia ofisini,.. Kitu cha kwanza alishangaa kukaribishwa utafikiri alikuwa akisubiriwa yeye...
"karibu... Karibu mwalimu"
Alishangaa mpaka akatukuzwa kwa cheo na kuitwa mwalimu,.. Alimshukuru mungu katika moyo wake, japo hajui kama atapa kazi, lakini kwa uchangamfu huo ulimpa matumaini ya kupata kazi,..
"ahsanteni sana ndugu zangu... Habari za kazi jamani"
"aah salama tu sjui wewe huko utokako"
"aahh namshukuru Mungu ni salama sana tu"
"basi in sha alah, karibuni sana"
"ahsante sana... Aahh naweza kumuona mkuu wa shule"
"ndio, bila shaka ni ofisi ile pale"
"Maashalah.. Kumbe ni pale tu"
"ndio Waweza kwenda kumuona"
"basi niwashukuru kwa hilo"
"haya haya"
Basi suria alitoka pale staff kisha akaenda kwenye ofisi ya mkuu wa shule hiyo,...
"hodi hidi"
Suria alibisha hodi huku akigonga mlango kiaina hivi"
"karibu"
Alikaribishwa na sekretari, kisha akaketi...
"ahsante"
"Samahani, nikusaidie nini"
"aahh Samahani dada.. Nina shida na mkuu wa shule"
"ok una miadi nae"
"mmhh hapana.. Kiukweli ni binafsi zaidi"
"ok wacha nimpigie simu"
Basi dada yule alipiga simu kwa mkuu wa shule, ambaye yupo chumba cha pili, ila huezi kumwona mpaka uwe na miadi nae..
"amesema ingia"
Suria alifurahi kuruhusiwa kuingia,... Lakini sasa ndani ya hicho chumba, alionekana maimati kasimama katika kona ya ukuta,.. Lakini hakukuwa na mwenye uwezo wa kumwona pale alipo...
"Shikamoo mzee wangu"
"marahaba kijana habari yako"
"salama tu... Aahh Samahani mzee wangu,. Nimekuja katika shule yako, ili niweze kupata nafasi ya uwalimu"
Aliongea suria akimaanisha kuomba kazi,..
"hebu tuone vyeti vyako"
Suria bila wasiwasi alitoa vyeti vyake,.. Mkuu wa shule kuangalia, duuu suria ni bonge la msomi, yaani ni msomi atari...
"aahh kijana.. Familia yako iliwekeza sana kwenye elimu yako"
"ndio mzee wangu... Kiukweli nawashukuru sana wazazi wangu kwa hili"
"ni kweli, pongezi zao... Lakini kijana.. Kiukweli hapaaa... Nafasiiii ha.."
Mkuu wa shule alitaka kusema nafasi za kazi hakuna, lakini kabla hajasema hivyo.. Maimati alimulika mwanga mkali katika kichwa cha mkuu wa shule...
"hebu subiri kidogo..... Batuliiii"
"yes boss"
"njoo"
Aliitwa batuli ambaye ndio sekretari wake, na huyo ni sekretari wa mkuu wa shule, na sio sekretari wa shule
"ndio boss"
"hivi mwalimu saidi toka alipotoka juzi alirudi kweli"
"hapana.. Tena aliondoka kwa matusi sana,.. Kiukweli hawezi kurudi"
"anhaaa... Basi kaendelee na kazi zako"
"sawa boss"
Batuli aliondoka na kwenda kuendelea na kazi zake,.. Kisha mkuu huyo mwenye umri mkubwa sana akaanza kuzungumza na suria...
"una bahati sana... Hebu barua yako ya maombi ya kazi"
Suria alitoa barua ya maombi ya kazi, na kumpatia mkuu wa shule...
"una hati nzuri sana..."
Aliongea mzee huyo huku mlango ukifunguliwa na akaingia batulia
"enhee nini tena"
"boss..kipindi cha masomo ya dini kimefika"
"mwalimu huyu hapa.. Mchukue ukamwonyeshe kila hatua na anaanza kazi leo leo huyu... Kijana.. Mfuate batuli akakupe mikakati ya kazi"
Ilikuwa kama bahati japo maimati kahusika kwa namna kubwa katika swala la suria kupata kazi,.. Hii shule ina tabia, mwalimu akiacha kazi.. Basi ule mshahara wake huliwa na mkuu wa shule, sasa hakutaka kuleta mwalimu mwingine kwani walipo Wangeweza japo hawana taaluma ya kumudu somo la dini japo ni shule Kiislamu lakini sio kuwa inafundisha dini, bali na masomo aina yote yanayo fundishwa kwingine hata hapa yanafundishwa... Na kila mmoja ana kipindi chake kila darasa
Suria hakurudi nyumbani siku hio kaanza kazi, tena kaanza katika darasa la wanafunzi wa kidato cha nne,... Hapo ni somo la dini, na akitoka hapo anakwenda kidato cha tatu vivyo hivyo mpaka afikie kidato cha kwanza ndipo anakwenda nyumbani... Na somo lake ni hilo tu
Islamic Knowledge, mana suria emesoma na akasomea sekta hio...
Katika darasa hilo, dawati la mwisho kabisa ambalo halina mwanafunzi.. Alikuwa kakaa maimati, lakini hakuna alie muona na wala hakuna atakae muona, mpaka aamue mwenyewe kuonwa na binadamu, na hata ukimuona utamuona kama binadamu wengine, hivyo bado hutojua ni jini..
Suria akiwa yupo bize na ubao, tena hakaukwi na maneno mana sifa ya mwalimu ni kuwa mwongeaji na wanafunzi wako...
"kamwalimu kadogo eee"
Aliongea mmoja wa wanafunzi walipo jirani na maimati...
"Afadhali huyu... Kuliko lile lizee"
Aliongea mwanafunzi mwingine, na mwingine akadakia na kusema
"afu ni hensam"
Sasa mwanafunzi huyo aliposema kuwa suria ni hensam, maimati alishtuka sana..
"ina maana hii shule haina maadili kwa wanafunzi?.. Inakuwaje wanafunzi kuanza kumtamani mwalimu wao"
Aliongea maimati lakini ni katika moyo wake,...
"haya sasa wanafunzi wangu, wadogo zangu,.. Nilianza na mbwembwe za ubaoni ili muone uwezo wa Mwalimu suria... Naitwa suria, ila nyie nitawajua taratibu.."
Aliongea suria huku akitabasamu, sasa kumbe tabasamu lake limekuwa haluwa kwa maimati... Huezi amini maimati naye alikuwa akitabasamu zaidi...
"mwalimu ana tabasamu zuri"
Aliongea fadhila ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne,
Saaa fadhila kumwangalia Mwanaidi, kamkuta amelegeza macho zidi ya suria....
"we Mwanaidi"
"nini bwana fadhila.. Tunakatiana stimu"
Yaani walikuwa katika somo la imani lakini wao hawaelewi,.. Kisa uzuri wa suria..
"Mwanaidi, ina maana ushampenda ticha suria"
"pigia mstari... Now is your brother-in-law"
"haaaaaaaaaa, mwanaiiiiiiiidiiiiiiii"
Sasa maimati kawaangalia sana hawa wasichana, akajua hapa kamsaidia suria sehemu ambayo sio ya maadili yake... Akajikuta kakosea sana na anajuta kumsaidia suria kwenye hii shule... Lakini sasa hakukua na jinsi,.. Pale pale maimati kaivua pete yake ambayo ilikuwa na urembo wa kike na ni pete ya dhahabu ila ina urembo wa kike... Aliivua kisha akairusha pale mbele alipo suria... Na hakuna alie ona, na hata suria hajaona wala kusikia mshindo wa kitu kikidondoka.. Mara suria akadondosha chaki, sasa ile anainama tu, akaiona ile pete... Hakuigusa lakini akatoa tangazo...
"wanafunzi wangu... Kuna mmoja wenu kadondosha pete yake hapa"
Aliongea suria huku akiendelea kuandika, wala hana muda nayo mana anajua ni ya mwanafunzi wake
"heee... Amesemaje yule hensam"
"we fadhila, hebu Jieshim.. Ile pete anataka anipe mimi kwa njia hio.. Sasa wewe wataka kujua ili iweje"
"kwani wewe umekuja na pete wewe"
"si nimekwambia anataka anipe"
"lakini Mwanaidi... Mwalimu kaanza kazi leo.. Ushaanza kumtamani jamani"
"weeeee, najua hapa kuna mbwa mwitu, nikichelewa tu sina changu.. Si unakumbuka mwalimu Shabani.. Nilimpenda nikajifanya kuchelewaa.. Mpaka zaina akamchukua... Ina na hiyu nichelewe?? Hapana.. Wacha nikachukue Pete kama zawadi yangu toka kwake..."
"mmhhj haya mwaya"
"sio haya... Najua anaogopa kunipa mbele yenu mana kuna miaka 30 jela.. Hivyo ananipa kiujanja ujanja.. We si unaona hakuna aliotoka"
Aliongea Mwanaidi huku akinyanyuka kwenye meza yake kuelekea mbele ili kuchukua ile pete... Na wakati huo maimati anaangalia tu, Mwanaidi anavyokwenda kuchukua ile pete
Itaendelea...............