Njia Rahisi Ya Kuchukua Namba Kutoka Kwa Mwanamke Unayemjua


Kuchukua namba kutoka kwa mwanamke ni rahisi zaidi kuliko hata kutamka jina lako. Unachohitajika ni kuenda moja kwa moja kwa mwanamke unayetaka kumuomba namba halafu unamwagiza akupatie. Mara nyingi mwanamke hawezi kukataa kukupatia namba yake unless uwe umemuapproach kwa njia isiyofaa ama hakujui. 


Mara ya mwisho mimi binafsi nilichukua namba kwa mwanamke chini ya dakika moja ya kukutana na yeye. Nilikuwa nimeandamana na marafiki zangu halafu mwanamke mmoja akapita kando yetu halafu muda wa dakika nikaamua kumuaproach na kunipatia namba yake ya simu hapo hapo. 

Kama bado unatatizika ni njia gani za kuchukua namba ya simu kutoka kwa mwanamke basi fuata maagizo haya ya haraka ambayo nitakuelezea. 

#1 Jiamini.  Kujiamini ni kitu muhimu. Wakati unapoamua kuapproach mwanamke lazima uwe unajiamini. Utajiamini vipi? Kujiamini ni rahisi. Kile unachohitajika kufanya ni kuweka nia kuwa wakati ambapo utamwaproach mwanamke lengwa basi lazima namba yake ya simu atakupatia. Huko ndiko nikujiamini. 

#2 Kuwa na mawazo chanya.  Mawazo chanya ni mawazo ambayo yanakubaliana na wewe. Mfano unaweza kuwa unataka kufanya kitu, halafu katika akili yako umeweka dhana ya kuwa kile ambacho unakusudia kufanya basi kitafanikiwa. Haya ndio tunayaita mawazo chanya. Ni dhana ambayo unaamini kuwa itatokezea. Ukiweka mawazo chanya kuwa ukiapproach mwanamke flani na atakupa namba yake ya simu basi bila shaka utafanikiwa. Lakini ukiweka mawazo ya kuwa hautafanikiwa basi kweli hautafanikiwa. 

#3 Kuwa mwigo.  Wakati mwingine inakuwa vigumu kabisa kwa wanaume flani kuongea na mwanamke. Inakuwa vigumu zaidi kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Njia rahisi ya kutatua shida hii haraka ni kuigiza. Kuomba mwanamke namba haichukui zaidi ya dakika mbili, hivyo unaweza kuwa mwigo. Unaweza kuigiza vile rafiki yako anavyoomba namba ya simu ama unaweza kufanya mazoezi kivyako kabla kumuapproach mwanamke kumuomba namba ya simu. 

#4  Relax.  Wakati unapoach mwanamke lazima uwe umetulia. Punguza wasiwasi, toa kijasho chochote ambacho uko nacho, pumua kiutulivu na uondoe ubabaifu wowote ulio nao. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa umerelax utakuwa na nafasi nzuri ya kukumbuka mambo ambayo umeyapanga kumwambia mwanamke flani. Hivyo ni muhimu kurelax kabla ya kuchukua approach yeyote. 

 Njia nzuri ya kumuapproach mwanamke


Njia rahisi ya kuomba namba ya simu kutoka kwa mwanamke ambaye unamjua na anakutambua ni ile ya moja kwa moja. Ukimwona anatembea mtaani halafu wewe umesimama na marafiki zako, mwanzo hakikisha umefuata masharti tuliyoyaeleza hapo juu; jiamini, relax, mawazo chanya na mwigo. Nenda moja kwa moja na umwambie hivi: 

"Mambo Mamito. Niko na ishu flani nataka kukuambia lakini sahizi naona si wakati mzuri wa kukuambia... Nipatie namba yako ya simu nitakupigia simu usiku."

ama

"Mambo Mamito. Napatie namba yako ya simu nataka kukupikia simu jioni nikwambie kitu flani"

Hii ndio njia ya moja kwa moja. Mwanamke wa kawaida, ambaye anakutambua hawezi kukataa kukupatia namba yake ya simu. Mwanzo unaweza kuwa na bahati ya kuwa huyu mwanamke alikuwa inteested na wewe tangu kitambo lakini anashindwa jinsi angeweza kuwasiliana na wewe.

Kama ni mwanamke ambaye humjui na hakujui, basi ni vyema kwanza ujitambulishe ili akufahamu. Si lazima uchukue namba yake ya simu siku io hio bali unaweza kungojea muda mpaka mzoeane.

Wanaume wengi wanatatizwa na tatizo la kutojiamini na woga. Lakini naamini kama unaweza kutatua mambo hayo mawili basi kazi yako itakuwa rahisi.