NINI CHA KUANDIKA KWENYE UJUMBE WAKO WA KWANZA WA MESEJI KWA MSICHANA ULIEKUTANA NAE KWA MARA YA KWANZA ?
SOMA STORY FUPI YA MAPENZI YA KUHUZUNISHA YENYE MAFUNZO KWENU HASA HASA WAKINA DADA. NI STORY YA KWELI KABISA
"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile
nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu
likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani
kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu
mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya
kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga
lakini aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani
nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye
atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari
aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo
na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo
baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa
kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa
wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta
kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona
katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu.
Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na
tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na
maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno
moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima
hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule
aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha
yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu
alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na
maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu.
Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini
uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu
kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie
vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu.
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku
moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume
mwenzako
AMENITENDA HIVI!!!