NIKIWA NA MSICHANA NAMKINAI,HIVI NI PEPO AU TAMAA TU?

Kuna rafiki yangu yupo kwenye mahusiano na msichana wake kwa miaka saba tangu wakiwa sekondari mpaka leo wamemaliza chuo kikuu wanaendelea poa.
Mimi maishani mwangu sijawahi kuwa kwenye ahusiano kwa zaidi ya miezi sita
nikilala na mwanamke mara mbili au tatu hata kama angekuwa mzuri vipi namkinai na nitamfanya visa mpaka aniache natafuta mwingine nae hivyohivyo
kuna mmoja aliniweza akanikaba mpaka kivuli huyu nilikaa nae muda kidogo lakini miezi sita haikuchukua.
Wakati mwingine nikishawakinai nafuta nambazao utakuta ananipigia nikiuuuliza wewe nani anakasirika wakati angejua nimeshawafanyia wenzake kama ishirini sasa hilo ni pepo au ni kujiendekeza wengine wamediriki kutishia kujiua baada ya kuwa nao kwa muda mfupi wakitarajia ndoa lakini wakaambulia visa na kuachwa….
Wenye uzoefu nishaurini sipendi ila najikuta tuu….