MBINU ZA KUMFURAHISHA MPENZI WAKO MUWAPO FARAGHA

Hakuna mahali ambapo unaweza kufundishwa namna ya kumfurahi­sha mumeo au mkeo, angalau ki­dogo wazee wetu enzi zao walikuwa wanapelekwa jandoni na unyagoni, siku hizi unakuja kujifunzia ndani ya ndoa, yaani kama ni mechi ya mpira wa miguu basi unajifunzia kutuliza mpira na kupiga danadana uwanja­ni wakati wa mechi ambayo ni lazima ushinde.
Mapenzi ni sanaa, lazi­ma ukubali kujifunza na kuyatafuta maarifa ma­hali popote yalipo ili uwe bora, huyo uliyenaye unaweza kuwa unafanya kila kitu kwa ajili yake, unajitahidi kumuonye­sha upendo wa hali ya juu lakini kama hujui nini cha ku­fanya muwapo faragha ili afu­rahi, ni sawa na kazi bure. Ni kwa msingi huo ndiyo maana nikaamua tujadiliane mada hii kama inavyojieleza hapo juu.
MAANDALIZI YA KIHISIA
Jambo la kwanza ambalo una­takiwa kulifahamu, ni kwamba ili mume au mke afurahie tendo muwapo faragha, lazima awe ametulia kihisia. Haiwezekani mmetoka kukwazana kuhusu jambo fulani, hamjapata suluhu na kila mmoja ana hasira halafu ndiyo mnaingia uwanjani, hamu­wezi kufurahia tendo kwa mtindo huo na hii inawahusu wote.
Maandalizi mazuri ya tendo yanaanzia katika maelewano, mpokee vizuri kwa maneno yaliyojaa bashasha, kwa sauti ya upole, mbembeleze, mpeti­peti na msifie! Ukiikamilisha kwa ukamilifu hatua hii ya kwanza na ya muhimu, basi utakuwa tayari umeshamuingiza kwenye safari ya kuelekea kufurahia tendo.
Mnapokuwa eneo la tukio, hu­takiwi kuwa na papara! Lazima kwanza na wewe akili yako uitu­lize na badala ya kukimbilia ku­ingia mchezoni na kuanza kupiga mbizi kama mtu anayejifunza kuogelea, unatakiwa kwanza ku­tumia muda wa kutosha kupasha misuli moto.
Muda unaoshauriwa kitaala­mu, ni angalau dakika thelathini
ndani ya muda huu mfanyie yale mambo yatakayoamsha hisia zake za ndani, viungo vya mwili wako kama mikono, vi­dole, mdomo, masikio vinaweza kuzalisha hisia nzuri sana kama utakuwa unajua nini unatakiwa kufanya kwa wakati gani.
Narudia tena, epuka kuwa na papara za kukimbilia uwanjani, maandalizi ni muhimu sana kwani yatamuandaa mwenzi wako kimwili na kihisia. Ukiwa na uhakika kwamba maandal­izi yamefanyika kwa ukamilifu, sasa unaruhusiwa kuendelea na hatua kubwa na ya muhimu inayofuatia.
Katika hatua hii ambayo kimsingi ndiyo inayowaungani­sha, pia unatakiwa kuwa na uelewa juu ya nini cha kufanya na kwa mtindo gani, siyo un­aingia kwa papara kama un­akimbizwa, hapana. Hapa pia unatakiwa kujifunza zaidi ili kuhakikisha unaibuka mshindi kwa kumfikisha mwenzi wako kwenye kilele cha safari yake ya huba.