WANAWAKE WANABOREKA WAKIFANYIWA HAYA KITANDANI



– Wanaume wamejaa majisifu, hata awe anaumia kiasi gani atakaa ngumu eti kwa sababu “mwanamume ni kuvumilia”. Kumbe mle ndani anakatika maini Wanaume wanahofia sana kuonekana bwege chumbani. Wanasayansi wamefanya tafiti kadha na kuhitimisha kuwa wanaume wanaogopa sana kuachwa na mchumba na pia kudhalilishwa. Eneo moja ambalo wanaume wanahofia zaidi ni kuonekana duni kitandani. Wanatatizika kila wanapofikiria kuwa ustadi wao uwanjani ni wa ligi ya chini; kwamba hawawezi kukufikisha kileleni ilhali unawapa mahaba ya kutosha. Habari Nyingine: Hizi ndizo njia bora za kuongeza ladha katika mapenzi Itakuwa vyema kwako mwanadada kuhakikisha kuwa unamuondolea mpenzi wako mawazo haya ya kumfedhehesha. Chukua hatua zifuatazo:
1. Usimlinganishe na wengine Yawezekana umekuwa na mchumba mmoja tu, ama yeye ni wa mia moja! Kwanza, usithubutu kumtajia idadi hiyo. Pili, usimlinganishe hata chembe na hao wengine wa zamani isipokuwa tu kama yeye ndiye ameibuka bora kuliko wote!
2. Usimkashifu Hakuna aliye kamili; mpenzi wako atashindwa na mechi nyakati zingine. Usimuonyeshe kadi nyekundu, subiri mechi iishe ama aondoke kwa utaratibu. Siku ambazo itakubidi ujifanye umefika kileleni, acha iwe ni siri yako mwenyewe; kama wasemavyo, hakuna siri ya wawili! Utamfaa zaidi wakati wa mechi ukimuelekeza kwa upole, hatimaye atatinga bao! Habari Nyingine: Zingatia mambo haya 7 ili kumtosheleza mumeo (video) Utamu wa mapenzi ni kubadilisha mitindo na usukani.
3. Usiwe wa kupewa tu Mazoea hayana raha hususan iwapo mwanamume wako anachemsha kila mnaporejelea mtindo ule ule. Utamu wa mapenzi ni kubadilisha mitindo mara kwa mara, kubuni njia zenu za kipekee kulishana mahaba. Kumbuka kuwa hakuna bingwa kitandani, mara kwa mara chukua usukani umuonyeshe mambo mapya!
4. Usilete vita chumbani Chumbani ni pahali pa kujituliza, kufungua roho yako na kujumuika pamoja na mpenzi wako kuleta raha. Vita nje na uweke kando mabishano yoyote; vile vile, majadiliano yasiyohusu shughuli mnayotekeleza, kama kupanda kwa gharama ya maisha.